Mwanzo - MSME Financing Gateway
World

Lango la Fedha linaorodhesha vyanzo vya fedha, mashirika ya msaada wa biashara na washauri ili uweze kuchuja haraka, kuchagua na unganisha chaguzi za ufadhili na huduma za maendeleo ya biashara zinazolingana na mahitaji yako Soma zaidi

Jifunze kuperuzi kwenye mfumo wa MSME Financing Gateway

Jifunze ni kwa jinsi gani mfumo wa MSME Financing Gateway utakavyokusaidia kutafuta na kuunganishwa na watoa huduma za kifedha na wafadhili wa maendeleo ya biashara kwa kutumia vichujio na jinsi gani ya kuweka wasifu wa biashara yako ili kupata kwa haraka huduma zinazolingana na mahitaji yako.

Unachoweza kutimiza

  1. Orodhesha na linganisha aina mbalimbali ya mikopo inayofaa biashara yako, halafu udokeze mikopo inayolingana na biashara yako
  2. Tazama na linganisha taasisi kadhaa za kutegemeza biashara yako, zilizo na tajriba katika sekta ya biashara yako, na pia zinazotenda kazi biashara yako ilipo
  3. Soma zaidi kuhusu wafadhili na pia jinsi ya kuomba ufadhili
  4. Tumia stakabadhi mbalimbali kama vile Chuo cha ITC cha Biashara Ndogo
  5. Pata habari, matukio na ujumbe kuhusu ufadhili na huduma mpya za kukuza biashara
  6. Jisajili kama mfadhili wa biashara ndogo ama anayetoa huduma wa kukuza biashara. Waweza pia kuongeza au kubadilisha vidokezi vya biashara yako.
Another world

Harakisha ukuaji wako

Pitia kanzidata yetu yenye utajiri wa taarifa za huduma za maendelo ya biashara na mashirika ya usaidizi wa biashara. Tafuta inayolingana na mahitaji ya biashara yako katika eneo lako. Kanzidata yetu inajumuisha: Washauri wa usimamizi wa fedha, watoa huduma za mafunzo katika kuanza biashara, huduma za kihasibu, washauri, wakufunzi wa mikakati ya biashara pamoja na masoko,wafadhili, msaada wa kisheria, washauri wa biashara na washauri wa mambo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, taasisi za maendeleo endelevu na kukuza biashara ili kutoa uwezekano wa kuwa na biashara endelevu

Huduma za Kifedha

Mfumo wa MSME Financing Gateway unakupa orodha ya huduma za kifedha zinazopatikana kwa ajili ya wafanyabishara wadogo na wa kati. Unaweza kuchuja/chagua huduma zinazoendana na mahitaji yako na bofya kwenye ukurasa wa mtandao wa mtoa huduma au wakala ili kujua zaidi au kutuma maombi.

Kuna nini hapa

5 Nchi za Afrika Mashariki
239 Vyanzo vya huduma za kifedha na huduma za maendeleo ya biashara

Usajili wa kupokea majarida

Jisajili hapa ili kupata Habari, Matukio, na Jumbe/Arifa kupitia barua pepe au mitandao ya kijamii kuhusu uzinduzi wa machaguo mapya ya huduma za kifedha au huduma za usaidizi wa biashara, matukio na taarifa za ulaghai/utapeli.

Washirika

MSME Financing Gateway inaletwa kwako kwa udhamini wa:

Kituo cha biashara cha kimataifa (ITC) na Farwell Innovations, Nairobi wametengeneza mfumo huu wa MSME Financing Gateway ili kukabiliana na mahitaji kutoka kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati takribani 1000, watoa huduma za kifedha na wafadhili wa maendelo ya biashara waliofanyiwa utafiti mwaka 2020. Mfumo huu umetengenezwa, kujaribiwa, na kuzinduliwa kwa msaada wa kifedha kutoka umoja wa Ulaya (EU) kupitia programu yake ya MARKUP II. 

Mpango wa kuboresha ufikiaji wa masoko wa awamu ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (MARKUP II) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) umetoa msaada wa kifedha ili kutengeneza, kuzindua, kujaribu na kulipia gharama za awali za mfumo huu ili kupatikana mtandaoni. Kwa taarifa zaidi juu ya mradi huu tafadhalli tembelea: https://www.eacmarkup.org.

Umoja wa mabenki Tanzania (TBA) ni msimamizi wa wa mfumo huu wa MSME Financing Gateway nchini Tanzania ili kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha nafuu na za uhakika kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Tunawashukuru watu, mashirika, na taasisi mbalimbali katika eneo husika ambao wametoa michango katika kuunda na kutengeneza mfumo huu

support imageWasiliana nasi