Please ensure Javascript is enabled for purposes of website accessibility
World

Kuhusu Mtandao Wa Huduma Za Kifedha Kwa Wafanyabiashara Wadogo Na Wa Kati

Kuziba pengo kati ya wafanyabiashara (wadogo na wa kati), watoa huduma za kifedha, na watoa huduma za ufadhili wa maendeleo ya biashara kwa kutumia programu ya mtandao ili kuboresha uwazi wa taarifa.

Karibu kwenye MSME Financing Gateway

Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) kupitia ubunifu wa Farwell walitengeneza mfumo huu ili kukabiliana na mahitaji makubwa kutoka kwa maelfu ya wafanyabiashara wadogo na wa kati, watoa huduma za kifedha na wafadhili wa maendeleo ya biashara waliofanyiwa utafiti katika Afrika Mashariki mwaka 2019 na 2020. Mfumo huu umetengenezwa kwa msaada wa kifedha wa mpango wa pili wa kuboresha upataji wa soko wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (MARKUP II) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Kituo cha Biashara cha kimataifa (ITC). Usaidizi huu umetuwezesha kupanga, kuzindua, kujaribu na kulipia gharama za awali za kuwezesha mfumo kupatikana mtandaoni.

Another world

Hili ni toleo la kwanza la mfumo wa MSME Financing Gateway. Muundo ni matokeo ya hakiki kadhaa katika Afrika Mashariki na michango kutoka vyanzo vingi. Tungependa pia kutambua na kushukuru mashirika ambayo yamekubali kuandaa toleo la kwanza la MSME Financing Gateway kwa niaba ya jumuiya za wafanyabiashara wadogo na wa kati kote Afrika Mashariki.

Tutafanya kazi na taasisi za wasimamizi wa mfumo wa MSME Financing Gateway ili kuendelea kuboresha utumiaji, utendaji kazi na ukamilifu wa taarifa zilizopo kwenye mfumo wa MSME Financing Gateway. Tunakaribisha mapendekezo kuhusu jinsi ya kuufanya mfumo wa MSME Financing Gateway kuwa bora zaidi. Tafadhali tuma maoni au mawazo yoyote uliyonayo kwetu: info@tanzaniabankers.org kwa kuweka maneno "Financing Gateway" kwenye kichwa cha ujumbe wako.

Kwa niaba ya washirika wetu wote, natumai utafurahia kutumia mfumo wa MSME Financing Gateway.

support imageWasiliana nasi