Jua jinsi unavyoweza kufaidika kutoka kwenye mfumo wa MSME Financing Gateway
Bonyeza kitufe cha "Wasiliana nasi" chini kulia mwa skrini yako na ujaze fomu. Chaguo kichupo "Maswali ya kiufundi" na kumbuka kiungo ambacho hakifanyi kazi vizuri . Ongeza maelezo yako na ubofye kitufe cha "Wasiliana" ili kuwasilisha. Utapoke ujumbe wa uthibitisho. Kiungo kitaondelewa kwenye kurasa za umma hadi kifanye kazi ipasavyo.
Nyaraka/hati zinazohitajika kwa watoa huduma za kifedha au wawekezaji
Watoa huduma wote, waendeshaji wa shughuli za ufadhili na wawekezaji wanahitajika kukusanya angalau seti ifuatayo ya maelezo ya msingi kuhusu waombaji, au wanufaika wanaopata ufadhili wa Euro au Dola za kimarekani zaidi ya 2500 kwa mwaka:
Hati/Nyaraka muhimu zinazohitajika kwa mchakato wa awali wa utambulisho wa mteja (CIP)
Nini maana ya: Hati?Nyaraka za AML/KYC
AML: Kupambana na utakatishaji fedha
KYC: Jua mteja wako
KYB: Jua biashara yako (mteja)
Mchakato wa awali wa utambulisho wa mteja (CIP) ni hatua ya kwanza katika mchakato wa kumjua mteja wako (KYC) na huanza mteja anapotuma ombi la akaunti au la kupata huduma ya fedha. Ni sehemu ya 1 ya mchakato wa hatua 3 ya uwekaji wa huduma za fedha, watoa huduma za fedha na wafanyabiashara wadogo na wa kati kwenye mfumo wa MSME Financing Gateway.
Hatua ya 1: Kwa mjasiriamali
1. Kukusanya jina la mteja, tarehe ya kuzaliwa na anwani yake.
2. Kukusanya hati/nyaraka za utambulisho kama vile hati za kusafiria, leseni za udereva, vitambulisho vya mpiga kura na hata picha kwa ajili ya uthibitishaji wa kibayometriki.
3. Kuthibitisha taarifa hizi dhidi ya kanzidata za umma na mashirika mengine ya kuripoti wateja.
Hatua ya 1: Kwa maombi ya awali kwa biashara ndogo - Kila mnufaika anahitaji kutoa:
· Leseni ya udereva, hati ya kusafiria, vitambulisho vingine vilivyotolewa na serikali vyenye picha, kitambulisho cha kibayometriki, kama vile kwa kutumia jicho, alama za vidole au rekodi ya utambuzi wa sauti.
· Leseni ya biashara / hati/nyaraka za usajili.
· Hati za ushirika wa biashara na mukhtasari wa kikao cha wanahisa.
· Uthibitisho wa anwani ya biashara au ya makazi: Ankara ya matumizi, kadi ya bima ya biashara, kitambulisho cha mlipa kodi, taarifa za mkopo wa hivi karibuni au mkataba wa kupangisha/kukodisha.
· Taarifa za hivi karibuni za akaunti ya benki au ya mtoa huduma wa miamala ya fedha inayoonyesha jina la biashara na anwani iliyoonyeshwa kwenye hati/nyaraka nyingine.
· Barua ya utambilisho kutoka kwa ofisi ya serikali iliyo karibu nawe inayotambua kukufahamu na dhumuni la kufungua akaunti au kutuma maombi ya mkopo.
Hatua zinazofuata zinategemea kiasi na muda wa mkopo/ufadhili unaotarajiwa na ikiwa yeyote kati ya walio na maslahi katika hilo anaishi au anafanya biashara katika nchi nyingine. Mabenki na watoa huduma wengine pia wanalazimika kuangalia ili kuona kama wahusika au wamiliki wamewekewa vikwazo au wako katika uchunguzi.
Taarifa sahihi kufikia: Septemba 1, 2022,© Credit Suisse, Zurich, Switzerland
· Mfumo wa MSME Financing Gateway ni mfumo huria, mfumo wenye lugha zaidi ya moja na pia ni mfumo wenye usawa kwa vyanzo vya huduma za kifedha, taasisi za usaidizi wa biashara na washauri ambapo biashara/makampuni yanaweza kuchuja kwa haraka, kuchagua na kutumia ili kujiunganisha na chaguo za huduma za kifedha na huduma za ukuzaji biashara zinazolingana na mahitaji yao. Mfumo unaweza kupatikana kwa simu janja, kompyuta na Mac'.
· Mfumo wa MSME Financing Gateway unahifadhiwa na kituo cha biashara cha kimataifa (ITC) kwenye seva za umoja wa mataifa (UNICC) na kwa usaidizi wa sekretarieti ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Ulaya (EU), taasisi za maendeleo na uwekezaji kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati katika nchi husika, benki na vyama vya asasi ndogo za kifedha (MFI). Kila mfumo (MSME Financing Gateway) katika nchi husika unasimamiwa na shirika mwakilishi kwa nchi hiyo linalosimamia maudhui, picha, habari na matukio, rasilimali na viungo.
Mfumo huu pia hutoa habari na matukio, jumbe kwa huduma mpya zilizowekwa kwenye mfumo kwa watumiaji waliojiandikisha, viungo kwa vyanzo vya taarifa vya kitaifa na kikanda, ITC SME Trade Academy (Elimu Mtandaoni), Marejeleo ya haraka ya jedwali la uamuzi wa kupata huduma za fedha, upatikanaji wa huduma za fedha na miongozo ya kupata huduma za fedha kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kuna kiungo cha orodha ya wazi ya ITC E-ComConnect ya vikapu vya manunuzi (shopping cart) na watoa huduma za malipo (Payment Providers) kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaojihusisha na biashara ya mtandaoni.
· Mtazamo juu ya huduma zilizo nje ya mipaka: Watumiaji wa mfumo waliosajiliwa katika nchi moja waweza kupata taarifa, kuangalia na kuunganishwa na huduma za fedha, uwekezaji na maendeleo ya biashara za nchi nyingine shiriki katika mfumo huu.
· Watoa huduma za fedha na wafadhili wa maendeleo ya biashara watapata ripoti za uchanganuzi na njia ya moja kwa moja kuwafikia wateja waliokusudiwa, ambapo pia hupokea jumbe kwa huduma mpya, kuboresha kiwango cha ubadilishaji wa kuwa wateja.
Mkataba wa awali wa usaidizi wa kiufundi kwa nchi inayosimamia mfumo hudumu angalau miezi 12 baada ya "Uzinduzi rasmi wa mfumo" wa awali. Unaweza kuongezwa na taasisi inayosimamia mfumo katika nchi husika au na ITC ikiwa ufadhili wake unaruhusu.
Mkataba wa usaidizi wa kiufundi kwa sasa uko chini ya Farwell Innovations ya Nairobi na nakala itatolewa kwa wasimamizi wa mfumo. Mkataba huu unajumuisha muhtasari wa kiufundi kwa wafanyakazi walioteuliwa kusimamia shughuli za uendeshaji wa mfumo, kurekebisha "hitilafu", uboreshaji wa mfumo, hitilafu za utendajikazi wa mfumo, hitilafu za uendeshaji na mahitaji ya upatikanaji wa mfumo.
Usaidizi wa kiufundi wa TEHAMA kwa mfumo huu hutolewa na kituo cha kimataifa cha umoja wa mataifa (UNICC) kilichopo Geneva. Hii inafadhiliwa na ITC kadri ufadhili unavyoruhusu.
ITC inamiliki programu huria (Open Source) ya mfumo huu na hatimiliki yake.
Wafanyabiashara wadogo na wa kati 1000 waliofanyiwa utafiti na ITC na mashirika mengine kati ya mwaka 2020 na 2021 walisema kuwa kupata taarifa kuhusu marejesho ya fedha, huduma za kifedha au ushauri juu ya ufadhili wa biashara wakati wa UVIKO ni mojawapo ya vipaumbele vyao. Wajasiriamali wengi walijua chini ya watoa huduma saba wanaotoa huduma za kifedha mahususi kwaajili ya wafanyabishara wadogo na wa kati wakati kuna zaidi ya huduma 400 mahususi kwa ajili ya wafanya biashara wadogo na wa kati zinazopatikana kote Afrika Mashariki.
Benki zilisema kuwa zaidi ya asilimia 70 ya maombi ya kupata huduma za kifedha hukataliwa katika ombi la awali kwa sababu ya makosa katika uwasilishaji wa nyaraka/hati na kutokidhi vigezo vya msingi. Wakati huo huo maafisa mikopo hupoteza muda wa kujibu maswali mengi ambayo hayaendani na huduma zinazotolewa. Viwango vya ubadilishaji kutoka kwenye maswali yote yaliyopokelewa hadi kuwa wateja wa mkopo ilisemekana kuwa chini ya asilimia 30. Watoa huduma za kifedha na wafadhili wa maendeleo ya biashara walisema walitaka mfumo wa kuunganishwa moja kwa moja na jumuiya ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa huduma na bidhaa mpya.
MSME Financing Gateway imetengenezwa kukabiliana na changamoto hizi kwa kutoa mfumo unaotumia kiwango cha chini cha data (mtandao) na maudhui yanayomilikiwa, kusimamiwa na kuendeshwa na msimamizi wa mfumo katika nchi husika kwa ushirikiano na mabenki, watoa huduma za kifedha na wafadhili wa maendeleo ya biashara.
Msururu wa makundi lengwa katika nchi tano za Afrika Mashariki ulihusisha wafanyabiashara wadogo na wa kati, wakulima, mabenki, mashirika ya serikali, wadhibiti, jamii, watoa huduma za kifedha pamoja na wafadhili wa maendeleo ya biashara katika kubuni, kupata mahitaji ya utendaji wa mfumo, na majaribio ya toleo la awali.
MSME Financing Gateway imetengenezwa kwa msaada wa kifedha wa mradi wa EAC Market Access Upgrade (MARKUP) ambao unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na ITC na kuratibiwa na Farwell-Innovations Ltd ya Nairobi: https://www.farwell-consultants.com
MSME Financing Gateway inatoa njia ya moja kwa moja kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaotafuta huduma za kifedha na huduma ya ufadhili wa maendeleo ya biashara ili kukuza biashara zao.
Wafanyabiashara wadogo na wa kati hutumia mfumo huu kama mfumo-jumuishi ili kupata huduma za kifedha na ufadhili ambazo zitakidhi mahitaji yao na kuunganishwa moja kwa moja kwa watoa huduma za kifedha bila gharama.
Benki na watoa huduma wengine watapokea ripoti za mara kwa mara zinazohusu shughuli za watumiaji na taarifa za biashara ikiwa ni pamoja na taarifa za: kijiografia, idadi ya watu, sifa za biashara, mifumo ya utafutaji na mibofyo. Hii husaidia watoa huduma na watunga sera kutambua mahitaji ya huduma za kifedha, kipimo cha hitaji la soko, kufafanua mgawanyo wa soko, ofa na kampeni za uuzaji ambazo hazijafikiwa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Baada ya kipindi cha awali cha uendeshaji, watoa huduma waliosajiliwa wanapaswa kuwa na uwezo wa kutengeneza ripoti zao wenyewe.
Jumbe/Arifa za moja kwa moja hutumwa kwa waliojisajili kila wiki wakati huduma mpya za kifedha zinapochapishwa. Hii huwarahisishia watoa huduma kujaribu kwa haraka maoni ya wateja kwa huduma mpya katika toleo la mapema (Beta).
Wafanyabiashara wadogo na wa kati waliotaarifiwa na waliotayarishwa vizuri huongoza kwa viwango vya juu vya ubadilishwaji wa kuwa mteja & ufanisi kwa mkutano wa awali wa wakala na mteja. Wafanyabiashara wadogo na wa kati hupata taarifa kuhusu aina za huduma za kifedha, madhumuni yake, vigezo na nyaraka/hati zinazohitajika kupata huduma. Rasilimali zinazopatikana kwenye mfumo (MSME Financing Gateway) ni pamoja na jedwali la maamuzi la huduma za kifedha na maelezo ya athari za aina tofauti za mikopo, makubaliano na dhamana.
Hakuna kazi ya ziada kwa watoa huduma za kifedha au wafadhili wa maendeleo ya biashara: Violezo vya haraka, jumbe za moja kwa moja na vipeperushi katika upakiaji wa huduma za kifedha hupunguza muda unaohitajika kwa wafanyakazi wanaohusika na masoko pamoja na mawasiliano kuboresha au kuongeza huduma mpya.
Taarifa zinazotolewa huboreshwa kupitia vidokezo vya moja kwa moja vinavyotumwa wakati taarifa za mtoa huduma hazijabadilishwa kwa muda uliowekwa - kwa kawaida ni miezi 6. Huduma zitawekwa kwenye kumbukumbu ikiwa hakuna jibu litapokewa baada ya jumbe mbili za ukumbusho kutumwa kwenda kwa mtoa huduma.
Bofya kitufe cha "Wasiliana nasi" chini kulia mwa skrini yako na ujaze fomu. Chagua kichupo cha "Maswali ya Kiufundi" na kumbuka kiungo ambacho hakifanyi kazi vizuri. Weka taarifa zako na ubofye kitufe cha "Wasiliana" ili kuwasilisha. Utapokea ujumbe wa uthibitisho. Kiungo kitaondolewa kwenye kurasa zote za mtandao za umma hadi kifanye kazi ipasavyo.
Matoleo yote ya taarifa zilizoingizwa huwekwa kwenye kumbukumbu, na sio kufutwa. Wasiliana na msimamizi wa mfumo kupitia fomu ya "Wasiliana" iliyo chini ya skrini yako na ubainishe ni sehemu gani mahususi ya taarifa, huduma au akaunti inahitaji kurejeshwa.
Kila mtoa huduma ya fedha au mfadhili wa maendeleo ya biashara amepewa "Ukurasa wa Akaunti" kwenye mfumo wa MSME Financing Gateway. Hii ni akaunti yako binafsi, inayotumiwa kuunda, kuelezea na kuboresha taarifa kuhusu huduma zako unazotaka kuzionyesha kwenye kurasa za umma katika mfumo wa MSME Financing Gateway.
Hapa unaweza pia kuchagua orodha ya maneno ya vifafanuzi kutoka kwenye menyu yaliyounganishwa na maneno ya vichujio vya utafutaji na vichujio vya maneno muhimu kwenye ukurasa mkuu (Home Page) wa kurasa za mbele za mfumo.
Kabla ya kualika ushiriki wako, ITC na msimamizi wa mfumo katika nchi husika walikusanya taarifa za awali zinazopatikana wazi kwa umma kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi yako. Hii imeandaliwa ili kukusaidia mwelekeo wako wa awali na kufupisha mchakato wa uthibitishaji na kuboresha taarifa na kutupa kipimo cha juhudi zinazohitajika ili kuandaa uzinduzi wa mfumo huu. Unaweza kufuta, kuboresha au kuunda maudhui mapya kwenye ukurasa wa akaunti yako.
Ni wewe pekee, Msimamizi wa mfumo katika eneo lako, na ITC wanaoweza kuona ukurasa wa akaunti yako.
Watu walioteuliwa na taasisi yako kuboresha taarifa watapokea ujumbe ikiwa taarifa kuhusu huduma iliyo katika ukurasa wa akaunti yako haijakaguliwa au kuboreshwa ndani ya miezi sita tangu kuwekwa/kuundwa kwake. Ujumbe huo utarudiwa kutumwa kila baada ya wiki mbili. Ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa, ujumbe wa mwisho utatumwa kukujulisha kuwa huduma itawekwa kwenye kumbukumbu hadi taarifa zaidi toka kwako zitakapotolewa.
Mtu kutoka taasisi yako ambaye ameidhinishwa kupitia fomu ya uidhinishaji wa wafanyakazi wa uendeshaji anapewa ruhusa ya ufikiaji wa kurasa za akaunti ya taasisi yako kwenye sehemu ya nyuma ya mfumo (kanzidata) ili kufanya maboresho ya taarifa zinazoonekana kwenye sehemu ya mbele ya mfumo huu wa MSME Financing Gateway. Watu walioidhinishwa wanapaswa kuomba idhini zozote za ndani zinazohitajika kabla ya kuwasilisha maboresho yoyote kwenye mfumo huu wa MSME Financing Gateway. Msimamizi anaona maboresho yaliyofanywa kwenye Dashibodi yake na anaweza kuyakagua kwa haraka ili kubaini hitilafu za wazi za uchapaji au maudhui yenye nia ovu kabla ya "Kuchapishwa" na kuonyeshwa upande wa mbele wa mfumo ili watumiaji waweze kuona.
Mchakato wa hatua mbili umeundwa ili kuzuia maudhui yenye nia ovu kuonekana kwenye mfumo huu wa MSME Financing Gateway, lakini taasisi inayosimamia mfumo huu wa MSME Financing Gateway haiwezi kuwajibika kwa usahihi wa kiufundi au usahihi wa maudhui yaliyochapishwa na watoa huduma.
Taarifa imeorodheshwa kikamilifu, ikiwa na uainishaji wa lugha asilia na usaidizi wa utafutaji. Injini ya uchanganuzi hunasa vigezo vya utafutaji vilivyotumika, vichujio vilivyotumika, idadi ya mara ambazo maneno muhimu yametumiwa na mibofyo ya watumiaji. Ripoti hunasa idadi ya mara ambazo kila neno muhimu linatumiwa na mibofyo, ambayo inaweza kutazamwa kwenye wasilisho la "Jedwali".
ITC na taasisi inayosimamia mfumo huu katika nchi yako huziomba benki na watoa huduma wengine kukagua ripoti zao za uchanganuzi za Google au mtandaoni ili kufuatilia kile kinachotokea kwa watumiaji wa mfumo huu wa MSME Financing Gateway ambao hutembelea kwenye tovuti zao za mitandao - hii inaitwa "Ukaguzi wa asili (Origination Check)".
Maelezo haya yatasaidia kukamilisha ukaguzi wa matumizi ya mfumo na kuonyesha ikiwa maneno yaliyo katika vichujio yanaweza kuhitaji kurekebishwa ili watumiaji zaidi wapate huduma zinazolingana na mahitaji yao. Viashiria vinaweza kujumuisha:
- Mtumiaji anakaa kwa muda gani kwenye kurasa anazobofya,
- Je, watumiaji wanabofya zaidi na, ikiwa ni hivyo, kwa kurasa zipi?
- Je, wanaendelea kujaza fomu ya maombi, kufikia wakala, au hatimaye ombi la kupata mkopo likubaliwe kwa ukaguzi zaidi (ubadilishaji wa kuwa mteja umeanza)?
Orodha ya maneno ya vichujio inapatikana katika kila Mwongozo (Angalia kichupo "Miongozo ya Watumiaji") na pia hutumwa kwa watoa huduma wanapojiandikisha kwenye mfumo. Unaweza kutazama na kuhamisha menyu
Vifafanuzi ambavyo vinaakisiwa na maneno ya vichujio huchaguliwa kutoka kwenye menyu yenye machaguo mengi wakati kila aina mpya ya huduma ya kifedha inapoingizwa kwenye ukurasa wa akaunti ya taasisi yako kwenye sehemu ya nyuma ya mfumo huu (kanzidata).
ITC, taasisi inayosimamia mfumo huu katika nchi yako, chama cha umoja wa mabenki na wadau wengine wataandaa mapitio ya ukusanyaji wa taarifa na Mkutano wa kundi lengwa ili kukagua matokeo na kisha kurekebisha vichujio na vifafanuzi vilivyotolewa kwenye mfumo ili uonishwaji wa utafutaji kwa watumiaji, na pia utafutaji wa huduma uboreshwe - huu ni mchakato unaojirudia unaoitwa "Uboreshaji wa kiwango cha bei (Hit rate optimization)"
Mpangilio wa ripoti za uchanganuzi za watumiaji wa mfumo, shughuli za watumiaji wa mfumo huu na mibofyo kwenda kwenye tovuti za benki na tovuti za watoa huduma za fedha ni "Kazi Inayoendelea".
Katika miezi 3 ya kwanza ya operesheni kamili (Ufanyaji kazi wa mfumo wa MSME Financing Gateway). ITC, Taasisi inayosimamia mfumo na Chama cha mabenki watakagua taarifa inayopatikana kwenye mfumo, watatayarisha baadhi ya ripoti za awali na kuziwasilisha kwa watoa huduma kwa maoni na mawazo.
Baadhi ya miundo ya ripoti itatengenezwa na, mara tu idadi ya watumiaji wa mfumo itakapopanda juu ya kiwango cha juu kilichowekwa, tutaweka huduma ya kuweza kupatikana na kutuma taarifa ghafi iliyopo kwenye mfumo iliyoondolewa taarifa binafsi za watumiaji.
ITC itaunga mkono kampeni ya kutangaza mfumo huu wa MSME Financing Gateway katika kila uzinduzi wake ambayo itafafanuliwa na wadau na kuratibiwa na mashirika/taasisi za wasimamizi wa mfumo huu katika nchi husika, mashirika na taasisi nyingine katika nchi hiyo husika.
Baadhi ya shughuli hizi zitawekewa bajeti ndani ya fedha za mradi za ITC. Katika baadhi ya nchi mashirika ya serikali na mashirika yanayosimamia wafanyabiashara wadogo na wa kati hutoa michango ya aina aina kwa ajili ya ukuzaji/uboreshaji na utangazaji wa mfumo huu. Ukuzaji unaweza kuunganishwa na shughuli nyingine za kikanda/kitaifa.
Ripoti za uchanganuzi na utambuzi zitachapishwa na msimamizi wa mfumo huu katika nchi husika. Baada ya miezi sita au mwaka mmoja, kumepangwa kuwepo kwa tukio la wazi lenye lengo la kuwasilisha matokeo hadharani na kuunda kamati ya usimamizi ya kikanda au kimataifa kwa ajili ya kusimamia mustakabali wa mfumo huu.
Katika Sheria na Masharti (ToR) ya taasisi zinazosimamia mfumo huu kuna kifungu kimoja kinachomtaka msimamizi wa mfumo asiuze taarifa binafsi iliyokusanywa kupitia mfumo huu.
ITC haipendekezi kutumia mfumo huu wa MSME Financing Gateway au miongozo inayoweza kupatikana kwenye kipengele cha "Rasilimali" kibiashara.
ITC inajadili kikamilifu uwezekano wa kupata ufadhili wa kimataifa na msaada wa wafadhili kuhakikisha kuwa gharama za kusimamia na kuboresha mfumo kwa siku zijazo zinalipwa. Nia yetu ni kwa mfumo huu kuendelea kutumika bila malipo kama "mfumo wa kimataifa".